Unajaribu watu wasahau drama yako na baby mama-Bien Sauti Sol amshambulia Eric Omondi

Muhtasari
  • Alisema kuwa wanamuziki wa humu nchini wanapaswa kujitahidi kumwiga mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleon
Bien
Image: Maktaba

Eric Omondi kwenye chapisho lake jipya zaidi kwenye ukurasa wa akaunti ya instagram alishiriki chapisho ambalo lilizua hisia nyingi kwenye mitandao ya kijamii.

Aliandika maelezo marefu kwenye ukurasa wake wa instagram akizungumzia jinsi wanamuziki wa hapa nchini walivyodunishwa endapo kutatokea tamasha wasanii wa kimataifa wanapotembelea nchi za Afrika.

Alisema kuwa wanamuziki wa humu nchini wanapaswa kujitahidi kumwiga mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleon.

Alikataa kutumbuiza baada ya kugundua kuwa watu waliotengeneza bango la mabango Wizkid alipotembelea walifanya taswira yake kuwa ndogo huku wakipanua ya wizkid.

Eric Omondi alilinganisha hali hiyo hiyo baada yake kushiriki bango ambalo lilitengenezwa hivi majuzi la Sauti Sol.

Aliongeza kuwa Sautisol ni kundi linaloheshimika ambalo limesimamia tuzo kadhaa kwa hivyo halipaswi kamwe kujikadiria kiasi cha kuwainua wasanii wa kimataifa.

Bien  Sautisol alikanusha madai hayo na kumkejeli Omondi akisema kuwa picha hiyo imechorwa tu.

Pia alimnyamazisha akisema kwamba anapaswa kuzingatia drama ya baby mama wake.

"Wewe ni mjinga sana. Hizi ni habari za uongo. Unafanya mambo mengi sana kuvuma. Nini tatizo? Unajaribu kuwafanya Watu wasahau drama yako na baby mama wako? Je, ni jambo gani unajaribu kuthibitisha kwa ujuzi wako mbaya wa photoshop? 😂😂😂," Aliandika Bien.

Baada ya Jose Chameleone kumpongeza Eric, Bien pia alijibu na kusema kuwa;

"Msimamizi mkuu wa mchakato lazima achukue jukumu. Sidhani kama wasanii wakubwa wa Kenya wanatumika kama wainua pazia

Walakini ikiwa msanii yuko juu lazima ajenge thamani hadi kiwango anachoandika. Hiyo haiwapunguzi kwa njia yoyote

Katika kazi yangu nimefungua na nimeandika kichwa. Katika sehemu zingine za ulimwengu ambapo sijulikani bado ninaweza kufungua. Hainifanyi kuwa msanii mdogo. Falsafa katika ujumbe wangu ndiyo inayonifanya nionekane, si yule ninayecheza kabla au baada yake."