logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Arrow Bwoy azua mdahalo mitandaoni baada ya kutangaza mipango ya kuwania ugavana 2022

Tangazo la Arrow Bwoy sasa linaongeza orodha ya watu mashuhuri wanaotaka kuwania viti tofauti

image
na Radio Jambo

Burudani13 November 2021 - 12:33

Muhtasari


  • Arrow Bwoy azua mdahalo mitandaoni baada ya kutangaza mipango ya kujiunga na siasa
  • Tangazo la Arrow Bwoy sasa linaongeza orodha ya watu mashuhuri wanaotaka kuwania viti tofauti katika uchaguzi mkuu wa 2022

Wanamitandao wameachwa na hisia tofauti baada ya msanii Arrpw Bwoy kutnagaza mipango ya kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Nairobi, katika uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Alitoa tangazo hili kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alisema hivyo na nikimnukuu

"Nairobi zoea. Gavana wako mapema...The future is now 2022 nayo nayo."

Tangazo la Arrow Bwoy sasa linaongeza orodha ya watu mashuhuri wanaotaka kuwania viti tofauti katika uchaguzi mkuu wa 2022 na kufuatia tangazo hili la Arrow Bwoy, wanamitandao kadhaa waliitikia huku baadhi wakimtakia kila la heri katika matarajio yake ya kisiasa.

Wengine walitangulia kumwambia ajikite kwenye muziki kwa kuwa hawezi kuingia kwenye siasa huku wengine wakisema kuwa mbio hizo tayari zimefungwa na huenda asimudu.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

thenaiboi: Headquarters iko pande gani. Niko uku kwa branch

azinacapri: Govana wa kanairo ni mjamoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

ambussi_Kiongoss: umesema usmame ata kama ni kwa miguu zote mbiliπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

wendo_mukina: Najua utasimama atakama ni kwa njiaπŸ˜‚

mr_kennedymanwah: , utawezana uimbaji na Siasa mkuu?? haya basiπŸ‘πŸ‘πŸ”₯

mr_mombasa: Uko serious unataka kuingia kwa debe 2022 Nairobi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

blackgoldbeiby: Heri ukule hizo pesa zako bro polepole juu naona ukiziaribu Bure coming 2022

tboyomuse: You can't saver two master at the same shugulikia Kwanza Nadia apate ball


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved