'Tabia zake ni zangu,'Vera Sidika azungumzia mwanawe

Muhtasari
  • Vera Sidika alifichua kuwa ingawa ana kijakazi, hajawahi kuruhusu mfanyikazi wake kumtunza mtoto wake
  • Vera alifichua kuwa yeye na mumewe huwa wanamtunza kifungua mimba wao Asia
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Vera Sidika ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wanafurahia safari yao ya kuwa mama, kwa mara ya kwanza.

Vera Sidika alifichua kuwa alichagua kuwa mama wa kudumu kwani miaka michache ya kwanza ya mtoto ni muhimu sana.

Vera Sidika alifichua kuwa ingawa ana kijakazi, hajawahi kuruhusu mfanyikazi wake kumtunza mtoto wake.

Vera alifichua kuwa yeye na mumewe huwa wanamtunza kifungua mimba wao Asia.

Mtoto Asia anaonekana kuwa mtoto mwenye bahati sana. Mtoto wa Vera kwa sasa ana wafuasi zaidi ya elfu hamsini kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo Vera hajawahi kuweka picha zozote za bintiye mtandaoni,Vera alidai kwamba binti yake anafanana sana na baba yake kimwili.

Hata hivyo Vera amefichua kuwa tabia za bintiye ni zake 100%.

Vera amefichua jinsi hasira ya mtoto wake inavyoweza kupanda kutoka kiwango cha moja hadi 100 ndani ya sekunde

"Asia huwa anafanya nyuso za kupendeza,yangu ya kupendeza ni ile ananung'unika ni nzuri sana, sijui huwa anazitoa wapi

Pia huwa anafanya uso akiwa amekasirika kwa kukuangalia na upande wa jicho,ukicheza na maziwa yake

Kwa maana matiti saa zingine huwa inatoka akiwa anazubaa, pia ana hasira za haraka, huwa inapanda kutoa asilimia 0 hadi asilimia 100, hayo yote ni DNA yangu," Aliandika Vera.