Diamond aonyesha mapenzi makubwa anayo kwa familia yake na Zari Hassan

Muhtasari

•Zari Hassan alipakia video na picha zilizoonyesha wakijiburudisha na wanawe pamoja na baba yao katika eneo moja la burudani na biashara  nchini Afrika Kusini.

•Diamond alionekana akiwa amebeba watoto wake wawili walioonekana kujawa na bashasha na kufurahia kipindi walichokuwa na baba yao.

•Aghalabu nyota huyo wa Bongo ameonekana kuwapenda watoto wake na Zari zaidi kuliko wengine wawili ambao alipata pamoja na Tanasha Donna na Hamissa Mobetto.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Diamond Platnumz na mpenzi wake wa zamani Zari Hassan wameendelea kuwa kielelezo kizuri cha ushirikiano mwema katika malezi kati ya wazazi waliotengana.

Licha ya ndoa yao kuvunjika zaidi ya miaka mitatu iliyopita, wawili hao wameendelea kuwa na uhusiano mzuri huku  Diamond akionekana kuwapenda zaidi watoto wawili ambao alipata pamoja na mwanasoshalaiti huyo kutoka Uganda.

Takriban wiki moja tu baada yake kutamatisha ziara yake ya muziki Marekani, nyota huyo wa Bongo alienda Afrika Kusini kutembelea watoto wake, Latiffah Dangote na Prince Nillan wikendi iliyotamatika.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Zari Hassan alipakia video na picha zilizoonyesha wakijiburudisha na wanawe pamoja na baba yao katika eneo moja la burudani na biashara  nchini Afrika Kusini.

Diamond alionekana akiwa amebeba watoto wake wawili walioonekana kujawa na bashasha na kufurahia kipindi walichokuwa na baba yao.

#Zari #diamond #boramedia

Zari pia alipakia picha iliyoonyesha familia hiyo ikila na kunywa pamoja kwa furaha. 

Aghalabu nyota huyo wa Bongo ameonekana kuwapenda watoto wake na Zari zaidi kuliko wengine wawili ambao alipata pamoja na Tanasha Donna na Hamissa Mobetto.

Ameonekana kufunga safari nyingi za kuenda familia hiyo yake iliyo Afrika Kusini ambako Zari Hassan anaishi na kufanya biashara kwa sasa.

Haieleweki vizuri iwapo Diamond angali anampenda mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Uganda ila ni wazi kuwa uhusiano wao ungali mzuri.