Kuwa single ni chaguo la mwanamke,mwanamume ni kitu rahisi kupata-Amber Ray asema

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti Faith Makau anayejulikana zaidi kama Amber Ray ametumia ukurasa wake wa Instagram kudokeza kwamba yuko single
Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Mwanasosholaiti Faith Makau anayejulikana zaidi kama Amber Ray ametumia ukurasa wake wa Instagram kudokeza kwamba yuko single.

Kulingana na sosholaiti huyo, madai ya baadhi ya wanawake kwamba wameshindwa kupata mwanamume si ya kweli.

Kwake, kupata mwanaume wa kuchumbiana ni jambo rahisi zaidi maishani mwake.

Hii inaweza kueleza kwa nini Amber Ray bado hajaolewa baada ya kutengana na mfanyabiashara wa Nairobi Jimal Roho Safi miezi michache iliyopita, ndoa ambayo ilikuwa na utata, hasa mapigano yasiyoisha na mke wa Jimal, Amira.

"Sijui ni nani anayehitaji kusikia hili lakini kuwa mseja(single) ni chaguo la wanawake, hakuna kitu kama vile hawezi kupata mwanamume. Mwanaume ndio kitu rahisi kupata 🤣," Amber Ray alidai.

Ujumbe wake ulipokelewa na hisia tofauti kutoka kwa mashabiki na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

agufaimali3: Amiraa umeskia?😂

ellah_daudi: Tell them good😂😍

akardi._: Go get one for u. The streets ain't belong to u no more

mkasimelissa: Talk girl. They should know that it's always about choices. 🙌

kolawoleabiola12: Sure you have been approach by lot of man each day but the main point is the choice is yours dear