'Sisi tutakupiga hatutakuweka kama wasanii,'Wacheshi wamwambia Eric baada ya kuwashambulia

Muhtasari
  • Kulingana na Omondi, wachekeshaji wa Kenya hawaonyeshi juhudi zozote za kuboresha sekta ya ucheshi

Baada ya kuwashambulia wanamuziki wa Kenya kwa kipindi cha takriban siku kumi zilizopita  akidai kuwa wamelala, Eric Omondi sasa amewageukia wachekeshaji wenzake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mchekeshaji huyo asiyepungukiwa na drama amedai wasanii wa Kenya wamekosa mwelekeo, ubunifu pamoja na maono.

Kulingana na Omondi, wachekeshaji wa Kenya hawaonyeshi juhudi zozote za kuboresha sekta ya ucheshi nchini na wanachosha sana.

"Kama kuna kikundi cha watu ambacho kimekosa mwelekeo, ubunifu na maono ni wacheshi. Hakuna bidii!!! Ni kundi linalochosha zaidi la watumbuizaji nchini!!" Omondi amesema.

Huku wachekeshaji wakitoa maoni yao kuhusu ujumbe na ushambuliaji wa Eric Omondi, walidai kwamba watamchapa.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

eddiebutita: Kumbafu sisi tutakupiga hatutakuweka kama musicians tutakupangia beating moja maridadi sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

bienaimesol: KIGEUGEU

mcatricky: This guy is suffering from chronic brand insomnia !

game_changers254: Nyamba ulale kama umechoka. @mcatricky ako InternationalπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

nasrayusuff: Sasa umetuanza???πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚aiii

mwendemacharia: In whose hands will everyone be safe

certified_gesum: Nimejitolea kuchekesha wachinessee mnipeleke uko😒❀️

ateimisatibrian: Alafu ukifika kwa wanasiasa nitakusaidia ju naona kazi ni mingi πŸ˜‚πŸ˜‚

chomba_wajesus: Ukimaliza utukujie sisi ma pastorπŸ˜‚