Mama yangu alinilazimisha nimuite dadangu mkubwa-Mtumba man afichua haya

Muhtasari
  • Akiwa kwenye mahojiano, Sande alisema kwamba maisha yake ya utototoni hajwahi lelewa na mama au kuhisi upendo wa mama
Mutuba man
Image: Hisani

Sande Mayua almaarufu Mtumba man amesimulia jinsi alikaribia kujiua miezi chache iliyopita baada ya kuwa maarufu ilhali hana pesa.

Amekuwa akivuma baada ya video fupi za yeye akiuza nguo za mitumba kuenea.

Yaliyokuwa na maana zaidi ni yeye akisema 'Ngara mpaka useme umepata mubaba.' na 'Nunua ya kukata msamaha.' 'nunua ya kuenda kumuona pasta.

Akiwa kwenye mahojiano, Sande alisema kwamba maisha yake ya utototoni hajwahi lelewa na mama au kuhisi upendo wa mama.

"Kile naweza kumbuka ni kuwa baba yangu alikuwa ananipenda sana, aliaga dunia nikiwa na miaka 5

Baada ya baba yangu kuaga mama yangu alienda kuishi Mombasa ambapo watu wa familia waliniambia kuwa alikuwa anafanya kazi ya kujiuza yaani malaya

Niliteswa sana na kupewa majina mengi nilipokuwa naishi na familia ya baba yangu, wakati ulifka na nikaenda kuishi na mama yangu mombasa

Mama yangu aliteseka sana, nakumuka tukitoroka Mombasa na kuenda kuishi Nakuru tukihepa madeni ya watu."

Aliedelea na usimulizi wake na kusema;

"Nilirudi tena kuishi na wazazi wa mama yangu, ambapo mama yangu alikuja kuishi Nairobi na dada yangu, nilipokuwa naja kuishi na wao nyanya yangu aliniambia napaswa kuita mama yangu dada yangu mkubwa

Mama yangu alikubali ni muite dada yangu mkubwa, na dada yangu alikuwa ananiita mjomba, kwa sababu alikuwa anataka kuishi tu na mwanamume ambaye baadaye waliachana

Kutoka wakati huo sijawahi muita mama yangu mama, lakini sasa naelewa, mimi huwa naomba sana na kuna sababu yangu kufika hapa

Kile naweza mwambia mama yangu aende kanisani na aombe msamaha, aokoke, mama yangu ni mama na ninajua kwamba kuna wakati utafika nikuite mama, sio wwatu wengi wanajua hadithi yangu na mama yangu, amepitia mengi sana," Alieleza Sande.

Hata baada ya kuwa maarufu, Sande alisema kwamba yuko maarufu nchini ilhali hana pesa.

"ushawahi kuwa maarufu au mashuhuri ila huna pesa, mama yako anaona hutaki kumsaidia na una pesa dada yako anaona tu hivyo, watu nyumbani wanajua na kufahamu uko na pesa kwa sababu wewe ni mtu mashuhuri

Kuuza mitumba kumebadilisha maisha yangu ata kabla sijafahamika sana nchini."

Huku akizungumzia changamoto za kazi yake alidai kwamba watu wengi wamekuwa wakimuita shoga ilhali yeye sio shoga.