Mama yangu hakuniamini nilipomwambiakaka yangu alinibaka-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Ni wazi kuwa wengi unyanyaswa kingono na watu wa karibu nao, familia,jamaa na ata rafiki wa karibu sana
  • Visa vya ubakaji na unyanyasaji wa ngono vimekuwa vikiripotiwa na kuongezeka kila kuchao nchini
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Ni wazi kuwa wengi unyanyaswa kingono na watu wa karibu nao, familia,jamaa na ata rafiki wa karibu sana.

Visa vya ubakaji na unyanyasaji wa ngono vimekuwa vikiripotiwa na kuongezeka kila kuchao nchini.

Lakini swali ni je waathiriwa huwa wanapata haki kweli?

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanamke mmoja alieleza jinsi ndugu yake mkubwa alimbaka, na mama yake kutomuamini baada ya kisa hicho.

Hii hapa hadithi yake;

"Ndugu yangu mkubwa alinibaka mara ya kwanza na kuambia mama yangu ila hakuniamini wala kutilia maneno yangu maanani

Alininyanyasa kingono kwa muda, lakini familia yangu haikuniamni wakati huo nilimwambia dada yangu ambaye alikuwa ameolewa kuhusu masaibu yangu na akanielewa

Nilipobarikiwa na kifungua mimba msichana, niliamua kuenda kumtembelea mama yangu, mtoto wangu alikuwa na miaka 7, ndugu yangu ule tu alinibaka, nilimpata akitaka kujaribu kumbaka mtoto wangu

Mungu naye ni nani nilimgonga na mti kwa kichwa, tuliporudi nyumbani mama yangu hakutaka maneno hayo yaende mbele, karibu nimuue ndugu yangu, mama yangu alikuwa amekasirika na akanifukuza na mtoto wangu." Alisimulia mwanamke huyo.

Je umewahi pitia kisa kama hicho na ulichukua hatua gani?