Mchekeshaji Eric Omondi aachiliwa huru, baada ya kukamatwa mapema siku ya Jumanne

Muhtasari
  • Mchekeshaji Eric Omondi aachiliwa huru, baada ya kumatwa mapema siku ya Jumanne
Image: INSTAGRAM.// ERIC OMONDI

Mchekeshaji Eric Omondi ameachiliwa huru saa chache baada ya kutiwa mbaroni.

Mchekeshaji  Eric Omondi alidaiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa alipokuwa anaongoza maandamano jijini Nairobi.

Msanii huyo asiyepungukiwa na drama aliripotiwa kutiwa mbaroni asubuhi ya Jumanne alipokuwa ameongoza kikundi cha vijana kuandamana nje ya bunge la kitaifa kurekebisha sekta ya muziki nchini.

Eric alikuwa ametoa wito kwa wasanii na waandishi wa habari washirikiane naye katika maandamano kuelekea bungeni kudai kuchezwa zaidi kwa sanaa ya Kenya na malipo bora kwa wasanii wakati wa tamasha.

Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa akivuma sana hivi karibuni anadai vituo vya burudani vicheze asilimia 75 ya muziki wa Kenya.

Baada ya mchekeshaji huyo kutiwa mbaroni hisia tofauti ziliztolewa na wanamitandao, huku msanii KRG akidai kwamba Eric hapaswi kutiwa mbaroni, kwani anapigania haki za wasanii.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instaram KRG aliwafahamisga mashabiki wake kwamba mchekeshaji huyo ameachiliwa.

OCPD wa kituo cha Central Adamson Bungei alisema Omondi alikamatwa kwa kusababisha fujo nje ya bunge.

"Hakuwa amefuata taratibu za kufanya maandamano. Hata hivyo tunampanga,” Bungei alisema.