Kuwa muangalifu kuhusu mtu unayemuahidi ndoa .Kuna watu ambao wanaingia katika maisha yako wakiwa na nia tofauti na watu wengi watakupa visa vya jinsi walivyokuwa waathiriwa .
Lakini kuna uchungu ambao hauwezi kutulizwa kwa mtu kusema pole . Uchungu wa aina hiyo ni kama anaopitia Jared .
Baada ya uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa miaka mitatu na hatima yake ikaonekana kuwa ndoa ya kudumu maishani ,Jared hakuwa na shaka kwamba mke wake atakuwa Stacy milele .
Iwapo ungemuambia kwamba miaka miwili ijayo hawangekua pamoja basi papo hapo angekuita adui mkubwa wa maendeleo yake .
Unaweza kufikiri kwamba unamjua mtu hadi wakati anapofanya jambo fulani kisha unagundua kwamba my friend humjui kabisa .
Can You imagine baada ya Jaredkumuoa Stacy katika harusi ya kifahari ,ghafla mpenzi wake alianza kubadilika tabia na kufanya vitu ambavyo havikueleweka .
Pindi Stacy alianza kupata shughuli ambazo hazikuwa katika mipango .mawasiliano kati yao pia yalianza kukatika na maneno matamu yaliokuwa ya kawaida kama vile I miss you na I love you yalianza kuwa nadra sana kutoka katika kinywa chake .
Jared aligundua kuna tatizo na kweli hisia zake hazikumsaliti .
Yamkini ilikuwa bayana kwamba Stacy alikuwa keshatekwa fikra na mtu mwingine lakini Jared alishangaa mbona basi asiseme wazi ili waachane rasmi .
Kumbe makubwa yalikuwa njiani yamemgonja Jared ! Stacy alikuwa kapendana naex wake wa kitambo Msichana bila aibu aliamka siku moja na kumuambia Jared kwamba ‘ You are not mature enough for me,but my ex is’ .
Kwake Jared ,yote haya yalikuwa kama ndoto lakini kwa kweli ndio ulikuwa mwanzo wa ngoma .
Hakuelewa ni vipi msichana ambaye wamekuwa naye katika uhusiano kwa muda huo mrefu na hata kufunga pingu za maisha naye anavyoweza kusema kwamba yuamtaka ex wake.
"Miezi minne baadaye aliniacha na kumrudia ex wake, nadhani alikuwa amenipenda kwa ajili ya pesa zangu
Kwa kweli sikuelewa jinsi alivyoniacha ata baada ya kupitia mengi naye."