Mimi sio mtakatifu, naamini nalindwa na roho mtakatifu,'Daddy Owen asimulia aliyopitia mwaka mmoja uliopita

Muhtasari
  • Msaniiwa nyimbo za injili Daddy Owen amefunguka kuhusu mambo ambayo amekuwa akipitia tangu alipotengana na mkewe takriban mwaka mmoja uliopita
  • Aliendelea kunakili ujumbe wake na kusema kwamba anajua yeye sio mtakatifu
daddy owen
daddy owen

Msaniiwa nyimbo za injili Daddy Owen amefunguka kuhusu mambo ambayo amekuwa akipitia tangu alipotengana na mkewe takriban mwaka mmoja uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki huyo amesema jambo hilo lilimfungulia milango ya hisia tofauti ambazo zilimfanya apatwe na msongo wa mawazo.

Owen amesema yaliyotokea yalimfanya ajiulize maswali mengi na afanye mambo mengi yasiyo ya maana almradi tu ajithibitishie kuwa angali mwanaume.

"Wakati kama huu mwaka jana nilipata ufunuo.. ufunuo ambao ulibadilisha maisha yangu milele! Huo ulikuwa mwanzo wa hali ya kuhamaki, jambo ambalo lilinichanganya akili

Nikiangalia nyuma ni kitu ambacho bado siwezi kuelezea, ninachojua tu ilikuwa mwanzo wa kitu maalum.. vile vile, katika kipindi cha mwaka 1 nimepata mafanikio mengi! Nimegusa na kubadilisha maisha kupitia kazi yangu ya kibinadamu na kubwa zaidi kujenga Nyumba ya Watoto kwa watoto waliozaliwa na ulemavu.

Na hatua nyingine kuu imekuwa kurejea studio na kuja na albamu na kuizindua! Kwa mwaka mzima nimekuwa mshtuko wa kihemko! Kuishi peke yako kulifanya iwe ngumu zaidi! Kunifanya nijiulize maswali mengi!"

Aliendelea kunakili ujumbe wake na kusema kwamba anajua yeye sio mtakatifu bali anaongozwa na roho mtakatifu.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa hajashiriki tendo la ndoa na mwanamke yeyote katika kipindi hicho licha ya kuwa ndoa yake ilisambaratika.

"Je, ninajivunia? HAPANA! Nilijisikia vibaya na nilitishika, chochote kuhusu mimi kutaniana au kitu chochote cha aina hiyo ni kwa sababu niliathirika  kihisia ... nilikuwa na mashaka juu yangu mwenyewe! Je, niliomba msamaha kwa watu wanaohusika? NDIYO! Je, nilitubu na kumwomba MUNGU msamaha? NDIYO! Nimevuka mpaka??Je, nilikula tunda? (Najua wengi wenu mnataka tu kujua sehemu hiyo..) HAPANA! Sikula tufaha lolote .. bado natumia android!. Je, mimi ni Mtakatifu? Je, mimi ni mtakatifu kuliko wewe? HAPANA KABISA! Ina maana nina nguvu? HAPANA! Naamini ninaongozwa na kulindwa tu na ROHO MTAKATIFU! Kwa kweli dhambi ingetaka kukuondoa lakini kadiri ninavyoomba na kukaa katika NENO ndivyo ROHO MTAKATIFU ​​anavyopigana vita vyangu" Amesema Daddy Owen.