Njia moja kuu ya kudumisha ndoa ni kudumisha uaminifu-Msanii Vivianne asema

Muhtasari
  • Vivian alisema kuwa kitu pekee ambacho kimewaweka pamoja kwa miaka mingi ni uaminifu na mapenzi ya kweli
Vivianne na Sam West
Image: Maktaba

Vivian na Sam West ni miongoni mwa wanandoa maarufu nchini Kenya. Wawili hao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka mitano na wamefanikiwa mambo kadhaa pamoja.

Vivian alishiriki picha moja wapo walipokuwa bado wapenzi wachanga. Hii ni miaka kadhaa nyuma, wakati Vivian alikuwa bado sio maarufu.

Vivian alisema kuwa kitu pekee ambacho kimewaweka pamoja kwa miaka mingi ni uaminifu na mapenzi ya kweli.

Karne hii ya sasa wanandoa wengi wamepeana talaka sababu kuu ni kutoaminiana katika uhusiano wao.

"Mimi na Sam bado tunafahamiana.. miaka mingi baadaye.. Njia moja kuu ya kudumisha ndoa ni kudumisha uaminifu..

Wakati mwenzi wako yuko wazi na mwaminifu kwako heshimu uaminifu huo. Usitumie taarifa hizo na watu wengine isivyofaa na pia usitumie taarifa hizo dhidi ya mpenzi wako," Aliandika Vivianne.