- Aliyekuwa Meneja wa Tanasha Donna afichua aliyoyapitia Tanasha baada ya kuachana na Diamond
African Castro, aliyekuwa meneja wa Tanasha Donna alisema kuwa mama huyo wa mtoto mmoja alipaswa kutafuta usaidizi wa kitaalamu baada ya kuachana na Diamond.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Presenter Ali, Castro alisema kutengana huko kulifanya Tanasha kukosa mwelekeo.
"Drama ya uhusiano uliathiri kasi tuliyokuwa nayo. Ukweli ni kwamba Tanasha aliumia baada ya kuachana na Diamond na hakupumzika kutafuta msaada kutoka kwa mtaalamu
Hapo ndipo niliponawa mikono yangu na kumuacha kwa meneja wake mwingine. Nilikutana na Tanasha alipokuwa mwanamitindo," Alio ngea Castro.
Aliongeza kuwa Tanasha amepitia mengi, na kuwa hawezi andika kitabu bila kumtaja Castro.
"Alifanya Tangazo na Safaricom na ndipo alipojulikana, baada ya hapo akaenda NRG,Kuna mengi ninaweza kusema juu yake na kuna mengi anaweza kusema kunihusu lakini tuliamua kutoyazungumza
Amepitia mengi. Unachokiona sasa ni athari yangu. Hawezi kuandika kitabu bila kunitaja."
#presenterali #tanasha #tanashadonna