logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakwe wangu walimtafutia mume wangu mke mwingine-Kipusa asimulia masaibu ya ndoa yake

Kulingana naye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 8 lakini, sio ndoa ambayo alitamani alipokuwa msichana.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri23 November 2021 - 12:12

Muhtasari


  • Mwanamke asimulia masiabu ya ndoa yake, yaliyosababishwa na wakwe wake

Ndoa  ukiwa nje huonekana kuwa kitu kizuri sana na  hakuna mabaya huweza kutabiri au kujua baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kuleta msukosuko katika uhusiano kati ya  mume na mke .

 Wakati watu wanapofanya mipango ya kufunga pingu za maisha ,wengi hujua kwamba basi wamefika mwisho kuhusu  kuwahi kumtafuta mtu mwingine wa kuwahi kuishi naye maisha yao yote

Wengi wakati huo wa mwanzo mwanzo huwa hawafikirii kwamba  wakati mwingine kuna sababu au watu wengine ambao huweza kuwa na  ushawishi mkubwa wa kutengeza ama kuvunja ndoa yao .

Kuna wale wamepatana na wakwe ambao wanawapenda ilhali kuna baadhi ambao hawawezi kusikizana na wakwe wao kwa njia moja au nyingine.

Huku nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na mwandada anayeefahamika kama Benedicta, ambaye alinisimulia masiabu ya ndoa yake tangu alipofunga ndoa na mume wake mpendwa.

Kulingana naye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 8 lakini, sio ndoa ambayo alitamani alipokuwa msichana.

Benedicta ambaye ana watoto 2 anasema kwamba alaichana kusikizana na wakwe wake punde tu alipoingia katik afamilia yao.

"Baada ya harusi yetu mama mkwe alinitusi sana na nikavumilia,kwani mume wangu anamsikiza maama yake sana yaani yuseme ni 'mamas boy'

Tumeng'ang'ana miaka hiyo yote,lakini baada ya kuja kuishi Nairobu na mume wangu, wakwe wangu walimtafutia mke mwingine ambaye kwa sasa anaishi kwa nyumba yetu mashambani

Sikuona kuwa mama kwe anaweza kuwa na usemi kuhusu ndoa yetu nilipomuaona kwa mara ya kwanza, aliniambia ni siwahi rudi kwake, na baada ya kumwambia mume wangu anapumbazwa na mama yake na kumuunga mkono

Sijui maisha yangu yanaenda vipi, kwani niko kwenye dilema, kile naweza sema ni kuwa ndoa sio safari rahisi kwa maana utapatana na changamoto nyingi kuliko mafanikio ukiwa na wakwe ambao hawakupendi kamwe," Alizungumza. 

Lakini swali kuu ni je nani wa kulaumiwa katika ndoa hii?

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved