'Nimeumia sana,'Willy Paul amjibu Sanaipei Tande baada ya madai alikataa kufanya collabo naye

Muhtasari
  • Anahisi kusalitiwa kuwa alikuwa shabiki wake maisha yake yote bado hawezi kumpa collabo
  • Ndiyo hajakamilika lakini ana uhakika kuwa hajawahi kumdhulumu kwani hata hawako karibu
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Siku chache zilizopitia Sanaipei Tande alifichua kuwa hawezi kufanya kolabo na Willy Paul.

Kwa kuwa kwake kufanya collabo na msanii kuna mambo mengi ambayo huwa anayaangalia. Ambayo Willy Paul anaweza kuwa hajakidhi sifa.

Willy Paul hata hivyo  kwenye mtandao wake wa kijamii na amemjibu Sanaipei kwa hasira akisema ni tabia hiyo inayowafanya wanaume 'kukimbia'.

Willy amesema amekuwa  akimsikiliza Sanaipei Tande na alikuwa miongoni mwa vipenzi vyake lakini leo mahojiano hayo yamemfikia na kuumizwa na maneno yake.

"MTAZAMO WA AINA HII NDIO INAFANYA MABWANA WANATOROKA..Yaani huyu Dada Sanaipe.. Nilikua namsikiliza, alikuwa miongoni mwa wasanii bora kwa list yangu ya favorites lakini leo ndio haya mahojiano yake yamenifikia na kuniumiza sana

Kuwa shabiki wa mtu karibu maisha yangu yote alafu hivi ndio mtu anaongea? ndio mimi sio kamili lakini wewe sijawai kukosea ata siku moja coz sikujui ivo..

nilipoona hii clip nimeona kama kuna chuki nyingi kutoka kwako. Nimewahi kukukosea nini? Nimefanya kazi na wasanii bora wa kike duniani na hawajawai kuwa na kiburi kama hiki dada yangu.

nimefanya kazi na alaine, nandy, size 8  na wote ni wakubwa kukushinda but hawajawai kuwa ivi jameni. Walai Nilitaka tu a taste of ur voice kwa #THEAFRICANEXPERIENCEALBUM kwa sababu naamini umebarikiwa na talanta vibaya sana."

Anahisi kusalitiwa kuwa alikuwa shabiki wake maisha yake yote bado hawezi kumpa collabo.

Ndiyo hajakamilika lakini ana uhakika kuwa hajawahi kumdhulumu kwani hata hawako karibu.

Lakini alipoona clips anazoweka ana uhakika aliona chuki nyingi zikimtoka. Lakini alitaka tu kumtaja baadaye katika Albamu yake inayokuja.

"Wewe ni mmoja wa nimeona bora kufikia sasa. nilifikiria ukona roho safi kumbe iko ivi? sasa hautakuwa kwenye albmu kubwa. kila mtu mwenye ako hapo ni mkubwa kukushinda

Lakini bado nilitaka kuwa na wewe hapo aki 😢 Wasanii wakenya tukiendelea ivi tutazidi kulia ati mara ooh play Ke music ooh hatuchezwi ooh nyonyonyonyo ooh nyoforithopieko!" Willy Paul Aliandka.