'Hongera nilikuwa nauliza utaoa lini,'Size 8 asema huku akimpongeza DJ Ruff

Muhtasari
  • Size 8 ampongeza DJ Ruff kwa kufunga pingu za maisha
  • Kulingana na msanii huyo wa Injili, anafurahi sana kwamba DJ huyo ameoa kwa sababu aliendelea kumsumbua kwa maswali ya lini atafunga ndoa
DJ Ruff na mkewe
Image: size 8/Instagram

Mcheza santuri wa nyimbo za injili, DJ Ruff ndiye mwanamume aliyeoa mpya zaidi mjini. Alishiriki picha nzuri kwenye tovuti zake za kijamii na mke wake mpya na walikuwa wazuri sana.

Wanandoa hao walipongezwa na watu wengi sana haswa marafiki mashuhuri ikiwemo msanii wa nyimbo za injili Size 8.

Kulingana na msanii huyo wa Injili, anafurahi sana kwamba DJ huyo ameoa kwa sababu aliendelea kumsumbua kwa maswali ya lini atafunga ndoa.

Anaendelea kutoa Utukufu kwa Mungu kwa kuwezesha Aliyekuwa mwandalizi-Mwenza wake wa TV kupata mke.

"A very big congratulations to my former TV Co-host @djruffkenya and your wife 😍❀️😘 nilikuwa na shinda nikiuliza ruff utaowa liniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ its finally here uuuuwwwiiii celebration glory to God!!!!," Aliandika Size 8.

DJ Ruff alifunga ndoa jana kwenye Windsor Golf katika sherehe ya faragha ambayo ilishuhudia mwaliko wa tukio pekee.

Maisha ya mapenzi ya mchea santuri huyo hayajakuwa mitandaoni ya kijamii, kwa hivyo ndoa yake iliwashangaza wengi.