'Wamelala kutushinda,'Eric Omondi awashambulia wasanii wa Uganda

Muhtasari
  • Eric Omondi awashambulia wasanii wa Uganda
  • Kisha akaendelea na kuandika juu ya jinsi anavyotamani kupeleka vichekesho vya Kenya hadi kiwango cha kimataifa
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Eric Omondi kwenye chapisho lake jipya zaidi kwenye ukurasa wa akaunti ya instagram alishiriki picha yake akiwa amevalia mavazi meupe.

Kisha akaendelea na kuandika juu ya jinsi anavyotamani kupeleka vichekesho vya Kenya hadi kiwango cha kimataifa.

Alienda mbali zaidi na kusema kuwa yeye ni rais wa burudani na yuko hapa kutajirisha sio Kenya tu bali kupanua juhudi kwa nchi za Afrika Mashariki hadi wote wanafikia kiwango cha kimataifa.

Aliongeza kuwa Uganda ndiyo nchi ambayo imelala linapokuja suala la burudani.

Alisema tangu miaka saba iliyopita, nchi hiyo bado haijafikia kiwango cha kimataifa tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki. 

"RAIS WA BURUDANI AFRIKA!!! Baada ya Kumaliza Kenya๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช. TUNASAFISHA na Kuamsha AFRIKA MASHARIKI, Kisha TUNASUKUMA BARA. Hiyo ni KAZI ya RAIS YOYOTE. Kama UKWELI USEMWA, UGANDA IMELALA USINGIZI. Wanafanya MBAYA kuliko SISI. HIT ya mwisho ya PROPER International ninayokumbuka kutoka UGANDA ilikuwa Valu Valu by the GREAT LEGEND(RESPECT)@jchameleon na hiyo ilikuwa MIAKA 7 ILIYOPITA๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ BANGE UGANDA๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคฆโ€โ™‚๏ธ ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ," Aliandika Eric.

Wanamtandao waliitikia chapisho hili huku wengi wao wakikubali juhudi zake linapokuja suala la kuimarisha tasnia ya burudani nchini Kenya.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

jaden.vince.1: By the way uneza fanya comedy outside this continent ๐Ÿค”๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

a.mercy: Malizana na Kenya kwanza ๐Ÿ˜‚

iam_ibra.him: Utachapwa wewe.....nakuhurumia๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

vicmassluodollar: Uliza Besigye achana na hao watu

254_fineest: Wewe hujui Museveni ni nani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ hapangwingwi ๐Ÿ˜†