Wikendi iliyopita Mhubiri Lucy Natsha aliwaacha wengi wakimpongeza baada ya kufishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Carmel.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa aliyekuwa gavana wa Nairobi MIke Sonko alimuuliza Luch mbona hakumfahamisha alikuwa anachumbiwa.
Ni ujumbe ambao uliibua hisia tofauti mitandaoni huku,baadhi ya mashabiki wakiuuliza Sonko amfichue Natasha kama vile amaekuwa akiwafanyia wengine.
Wengi walidai kwamba awali wawili hao walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi,jambo ambalo Natasha alikana akiwa kweye mahojiano na Betty Kyalo.
Sonko alipakia video ya Natasha akiwa kwenye mahojiano ambapo alisema kuwa;
"Tulipiga picha hizo wakati gavana angali seneta na picha hizo ni za kitaalamu. Lakini watu daima watataka kusoma mambo jinsi wanavyotaka.
Kwa kweli, mkuu wa mkoa ni wa maombi sana na uhusiano wangu naye ni wa kiroho sana. Tumeomba pamoja kwa nyakati tofauti.
Sijawahi kudate na Mike Sonko, sijui hadithi hizo zilitoka wapi. Yeye ni mtu mwenye heshima sana, pamoja na yeye pia ana familia. Hizi ni uzushi tu."