'Ungeniambia fame itanilisha tungepigana,'Amberay afunguka kuhusu maisha yake ya awali

Muhtasari
  • Amberay afunguka kuhusu maisha yake ya awali
  • Ingawa Amber Ray anajulikana kuwa wakala au mpenda fujo, nyota huyo wa kike ameokoka na anamheshimu Mungu

Ingawa Amber Ray anajulikana kuwa wakala au mpenda fujo, nyota huyo wa kike ameokoka na anamheshimu Mungu.

Amber ana utu uliojaa ucheshi na pia anaweza kupendezwa ikihitajika au tuseme upande huo unapoamshwa.

Kutoka kuwa wa ajabu hadi kuwa mtulivu, yeye ni mchanganyiko wa mambo ambayo mtu hawezi kustahimili lakini kuburudishwa naye.

Katika chapisho la hivi majuzi ambalo alichapisha kwenye hadithi zake, nyota huyo wa kike ameandika machapisho manne akieleza jinsi anavyomwamini Mungu kupatana na kile Alichomfanyia.

Amber hakuwahi kutaka umaarufu kulingana na chapisho lake kwenye Instagram lakini hilo ndilo limemwezesha kupata riziki na pia kujilisha pamoja na familia yake.

"Miaka 8 iliyopita ungeniambia hii fame itanilisha one day tungepigana mbaya, lakini Mungu alikuwa na mipango yangu

Kwanza nikikumbuka vile nilipata umaarufu, wacha tuseme nilibatizwa na moto, hapana sijawahi tamani kuwa maarufu lakini sasa nafurahia maisha yangu niliyonayo sijafikia malengo yangu

Najivunia kwa kutokata tamaa, kwa kutojidharau na Mungu kutoacha upande wangu ata baada kuwa na machungu naye na kuacha kumuamini kwa yale niliyokuwa napitia wakati ule," Alisema Amber.

Amber amekiri kwamba wakati huo marafiki zake walimuacha na hata kumuumiza zaidi.

"Fikiria kujaribu maisha yako kuwa karibu na Mungu alafu ghafla wakati mgumu unakujia na badala ya kumuamini Mungu unaanza kumuuliza maswali

Nakumbuka pia nikimwambia kwaba anasema kwamba hawezi kukupitishia jambo ambalo huwezani nalo

Lakini kwangu nilihisi Mungu aliniamini sana , nilikuwa nakufa ndani ndani na hamna wa kumlilia, watu ambao nilikuwa natumia muda mwingi nao walinigeuka na kuniumiza mahali panauma sana

Unaposikia wakisema familia kwanza waamini kwani familia ndio nilibaki nayo."