Siwezi kukupa ulimwengu lakini nitakufundisha neno na njia za Mungu-Zari amwambia mwanawe

Muhtasari
  • Leo ni mtoto wake na Diamond Platinumz siku ya kuzaliwa ya Prince Nillan anatimiza miaka 5
Prince Nillan
Image: Zari/INSTAGRAM

Mwanabiashara maarufu na mwasosholaiti kutoka Uganda Zari Hassan maarufu kama Zari the boss lady anasherehekea siku ya kuzaliwa ya wanawe leo.

Ana jumla ya watoto 5, wavulana 3 kutoka kwa ndoa yake ya kwanza na marehemu Ivan Ssemwanga na wengine 2 mvulana na msichana kutoka kwa ndoa yake na mumewe wa zamani Diamond Platinumz.

Leo ni mtoto wake na Diamond Platinumz siku ya kuzaliwa ya Prince Nillan anatimiza miaka 5.

Zari alimwandikia mwanawe anda ujumbe mtamu wa siku yake ya kuzaliwa akisema,

 

'Heri ya kuzaliwa kwa Amigo mtukutu zaidi wa nyumbani, nina hakika kwamba hukujua hili, siwezi' siwezi kukupa ulimwengu lakini nitakufundisha neno na njia za Mungu, ukiweza kujifunza na kutawala kwamba ulimwengu utakuwa wako, Mungu akubariki kwa ajili yangu'.