Asante umeshinda,'Willy Paul amwambia Diana Marua huku akifichua amepoteza mikataba ya milioni 96

Muhtasari
  • Wawili hao wamekuwa wakishambuliana mitandaoni, huku wakizidi kuvua mitandaoni
  • Willy Paul afichua amepoteza mikataba ya milioni 96 baada ya madai ya Diana Marua
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Wiki iliyopita, Diana Marua, mke wa Bahati aliweka kwenye mitandao ya kijamii madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Willy Paul, na hatua hii ilifanya wanawake wengi zaidi kumpinga Willy paul na tuhuma sawa.

Wawili hao wamekuwa wakishambuliana mitandaoni, huku wakizidi kuvua mitandaoni.

Willy Paul ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusu hasara aliyoipata kutokana na madai ambayo Diana alitoa dhidi yake akiorodhesha mikataba mitatu kutoka kwa makampuni matatu tofauti ambayo amepoteza.

Katika sehemu ya maoni, Wanamtandao hawajamwacha Willy Paul wanaonekana wakiacha maoni makali.

Kulingana na Paul Diana atalipia hasara ambayo amepitia kwa ajili ya madai yake, huku akisema kwamba lazima afike mahakamani ili apate haki.

"Asante umeshinda, nimepoteza dili la thamani ya 10m kutoka kwa kampuni ya mawasiliano. 4m kutoka kampuni ya magodoro. Na mkataba wa kimataifa wa kurekodi na usambazaji wenye thamani ya 82m. Asante sana. Umeshinda," Aliandika Willy Paul.