logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Asante kwa kunipa zawadi bora-Phil amwambia Kate Actress huku akisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe

Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2017, na wako pamoja wakilea watoto wawili. watoto

image
na Radio Jambo

Yanayojiri15 December 2021 - 10:33

Muhtasari


  • Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2017, na wako pamoja wakilea watoto wawili. watot
phil-karanja

Muigizaji na mama  Catherine Kamau maarufu Kate  Actress ametumia kurasa ake za mitandao ya kijamii na kumsifu bintiye, huku akimtakia heri  njema siku yake ya kuzaliwa anapohitimu miaka 2 .

Wanamitandao walifurahia  kumuona 'Njeri' aliyekua mzima kwani mamake huwa hachapishi kwenye mitandao ya kijamii.

Kate alibarikiwa kupata mtoto wake wa pili na mtoto wa kwanza na mumewe Phil, mtengenezaji wa filamu na mwigizaji mwaka wa 2019.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2017, na wako pamoja wakilea watoto wawili. watoto

Kate amekuwa wazi kuhusu maisha yake ya zamani kwa umma, kwani hapo awali alifichua kwamba alipata mimba ya mwanawe wa kwanza wa kiume alipokuwa chuoni.

Huku mumewe akisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe pia alimshukuru mkewe kwa kumpa zawadi bora ulimwenguni.

"Mtoto wangu amefikisha miaka 2 leo @Kate_Actress asante kwa kunipa zawadi bora ulimwenguni nakupenda sana," Aliandika Phil.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved