logo

NOW ON AIR

Listen in Live

2021 imenifundisha kujifunza kutokana na makosa yangu- Makena Njeri

Makena alisema yote yalianza kwa kuacha kazi na kuanzisha kampuni yake ambayo sasa inafanya vizuri.

image
na Radio Jambo

Habari20 December 2021 - 06:24

Muhtasari


  • Makena alisema yote yalianza kwa kuacha kazi na kuanzisha kampuni yake ambayo sasa inafanya vizuri
  • Kuwa halisi ni moja ya mambo ambayo yamemsaidia kujipenda na kufanya kile ambacho moyo wake unapenda

Makena Njeri ambaye ni miongoni mwa watu mashuhuri wa Kenya waliotangaza hadharani kuwa wako katika jamii ya LGBTQ, amejitokeza wazi kusema kwamba 2021 imekuwa funzo kwake.

Makena alisema yote yalianza kwa kuacha kazi na kuanzisha kampuni yake ambayo sasa inafanya vizuri.

Aliendelea kwa kusema mwaka huu alijifunza kujipenda, na safari ya kujipenda haikuwa rahisi, kwa sababu ilikuja na changamoto nyingi.

Kuwa halisi ni moja ya mambo ambayo yamemsaidia kujipenda na kufanya kile ambacho moyo wake unapenda.

Makena pia alizungumza kuhusu kuwa mzungumzaji katika majukwaa makubwa, na jinsi nafasi zote kuu alizopewa za kumimina moyo wake zimempa ujasiri wa kutosha na kujiamini kuwa yeye mwenyewe. 

Pia ameweka wazi kwamba mwaka wa 2021 umemfunza kujiruhusu kuwa na dosari na kujifunza kutokana na makosa yake.

Makena amekuwa akivuma kwa muda baada ya kutengana na Ntalami.

Huku tukiwa tumebakisha siku 12 tu kukamilisha mwaka wa 2021, je umejifunza nini mwaka wa 2021 na matarajio yako ya mwaka wa 2022 ni yapi?

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved