Wakati mtu anakuitisha picha za uchi wako mpe block mara moja-Benjamin Zulu

Muhtasari
  • Kulingana na mshauri huyo mtu wa kawaida hawezi piga picha za uchi wake na kuanza kusambaza mitandaoni

Mshauri Benjamin Zulu, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashaui mashbiki wake dhidi ya kuwatumia watu picha za uchi wao.

Kulingana na mshauri huyo mtu wa kawaida hawezi piga picha za uchi wake na kuanza kusambaza mitandaoni.

"Nitumie picha yenye inapendeza, Tena  wakai mtu atakutumia picha za uchi wake au kukuitisha picha za uchi wako mpe block mara moja

Mtu mwenye akili timamu hawezi zingatia kamera yake kwenye sehemu za siri na kuanza kuzisamabaza picha kama hizo

wametawaliwa na ngono na wamepagawa na mapepo ya tamaa, hawahitaji mapenzi au uhusiano wanahitaji kufukuzwa na mtu anayekudharau kiasi cha kukushirikisha kwa njia mbaya na isiyo na heshima kamwe hawezi kukuthamini," Alisema Zulu.