Maneno hayawezi kukadiria upendo ambao umeonyesha,'Ujumbe wake Rachel kwa naibu rais William Ruto

Muhtasari
  • Leo ni sherehe mbili huku Rachel na Ruto pia wakiadhimisha siku ya ndoa yao
  • Ruto ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 55 na miaka 29 ya ndoa
  • Kupitia twitter, Rachel alimtaja Ruto kama rafiki wa kweli, msiri na baba wa ajabu kwa watoto wao
Naibu raiis William Ruto na mkewe Rachel Ruto
Image: Rachel Ruto/TWITTER

Huku naibu rais akiadhimisha miaka 55 ya kuzaliwa hii leo, wakenya na wanamitandao wameweza kumtumia jumbe za kumsifu na kumtakia siku njema.

Mkewe Rachel Ruto amemlimbikizia sifa tele kwenye ukurasa wake wa twitter na kumshukuru kwa kuwa naye maishani.

Leo ni sherehe mbili huku Rachel na Ruto pia wakiadhimisha siku ya ndoa yao.

Ruto ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 55 na miaka 29 ya ndoa.

Kupitia twitter, Rachel alimtaja Ruto kama rafiki wa kweli, msiri na baba wa ajabu kwa watoto wao.

"Maneno hayawezi kukadiria upendo na usaidizi ambao umeonyesha.Heri ya siku ya kuzaliwa, na Mswada wa Sikukuu njema. Nakutakia baraka nyingi za Mungu na mafanikio makubwa katika kila hitaji la moyo wako," Aliandika Rachel.

Huku akiendelea kuandika ujumbe wa kusherehekea au kuadhimisha miaka 29 katika ndoa, alisema kuwa;

"Siku hii milele inasalia kuwa maalum. Tunaposherehekea siku yako ya kuzaliwa na maadhimisho ya harusi yetu, naweza kusema kwa ujasiri, Ebenezer - Bwana ametuleta hapa. Wewe ni rafiki wa kweli, msiri na baba wa ajabu kwa watoto wetu."