Namshukuru Mungu kila siku kwa ajili yako,'Diana Marua amwandikia Bahati ujumbe wa kihisia

Muhtasari
  • Diana Marua amwandikia Bahati ujumbe wa kihisia
  • Kulingana na Diana, Bahati ndiye mwanamum ambaye anamuelewa na kuwa anamshukuru Mungu kila siku kwa kuwa katika maisha yake
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Msanii Diana Marua kupitia kwenye ukurasa wakewa instagram amemwandikia mumewe Bahati ujumbe wa ihisia anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kulingana na Diana, Bahati ndiye mwanamum ambaye anamuelewa na kuwa anamshukuru Mungu kila siku kwa kuwa katika maisha yake.

"Katika Siku hii, Mungu Alinipa Mume 😇 Binadamu pekee ambaye analingana kikamilifu na wazimu wangu

Ni mmoja tu anayenielewa, ambaye amenipenda sawa tangu siku ya kwanza nilipokutana naye. Ni mmoja tu ambaye huweka kila kitu kando ili kuhakikisha kuwa mimi hutangulia. Yule ambaye amehakikisha kuwa kila ninachogusa kinageuka kuwa Dhahabu.

Mpenzi, Hakuna mtu ambaye nimechumbiana naye amekaribia wewe. Namshukuru Mungu kwa ajili yako kila siku. Nimenyenyekea na kuheshimiwa kuwa mke wako, kuhusishwa na wewe na kuwa juu ya ulimwengu nikishika mkono wako."

Bahati nadhaamisha miaka 29, hii leo na amepokea jumbe kutoka kwa mashabiki wake wakimtakia heri njema siku yake ya kuzaliwa.

"Nina furaha kusherehekea mwaka wako bora zaidi pamoja nawe. Mwaka wa 29... Tunasogea karibu na mwaka wetu wa Bilionea 💃 Jambo bora zaidi ni kujenga Ufalme na wewe

Usiku huo wa kukosa usingizi, siku ambazo sijisikii lakini unanisukuma kuwa kila kitu ninachoweza kuwa.

Wewe ni nyota inayong'aa, almasi, hazina ... umefanya kila kitu kinachokuzunguka ing'ae na kwa hilo, naomba kwamba mwaka huu mpya uwe bora zaidi uliopata, BADO!!!! MUNGU, ASANTE KWA HUYU MTU," Diana Aliandika.

Licha ya wawili hao kupokea kejeli kutoka kwa wanamitandao wamezidisha mapeni yao kila kucha huku wakiwadhibitishia wanamiandao kwamba hakuna kitu kinachowazuia kung'aa.