'Nikizungumza ninaweza kuharibu maisha yake milele,' Mulamwah afunguka kuhusu kuachana kwake na Carol Sonie

Muhtasari
  • Mulamwah afunguka kuhusu kuachana kwake na Carol Sonie
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mcheshi maarufu David Oyando almaarufu Mulamwah amezua hisia tofauti kati ya mashabiki baada ya matamshi yake  kuhusu madai ya kuachana na Carol Sonnie.

Haya yanajiri baada ya shabiki mmoja kuuliza sababu kuu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo. Wakati akizungumzia suala hilo, mcheshi huyo alimpapasa mpenzi wake wa zamani.

Mulamwah alimjibu kwa ujasiri shabiki ambaye alikuwa ameuliza swali hilo, akisisitiza kuhusu suala ambalo Mulamwah hakufichua haswa ni nini kilisababisha uamuzi wa kikatili wa kutengana na Sonie.

Huku akiweka mwenyewe sababu hiyo, Mulamwah hata hivyo aliwaacha mashabiki na maswali mengi yasiyo na majibu kuliko hapo awali huku akieleza sababu ya uamuzi wake wa kutoweka wazi sababu hizo.

"Watu wengi wameniuliza swali hili lakini nachagua kutolizungumzia kwani nikizungumza naweza haribu maisha yake milele na kuathiri mdogo wetu pia

Wanaume unyamza ili kulinda mambo mengi sana, kumfichua hadharani ili kusafisha jina langu, mambo yatazidi kuwa mbaya zaidi, labda siku moja utakuja kujua nini haswa kilitokea 

Lakini sikuwa wazimu kufanya uamuzi ambao niliufanya, wanaume huwa hawaendi tu," Mulamwaha alisema.

Uhusiano ni mtamu na mojawapo ya hisia bora zaidi ulimwenguni wakati wawili wanapendana.

Hisia hii inaonekana zaidi kwani wale wanaopendana wanaweza kuendelea kutuma mapenzi yao kwa maneno matamu ya maoni na manukuu.

Pia huwa mbaya pale wapendanao wanapoamua kuachana huku wengine wakiamua kufichua baadhi ya siri za wapenzi wao wa zamani.

Hii inaweza kusababisha kuchafuliwa kwa jina la Wapenzi wao kwa umma.

Mcheshi huyo pia aliweka wazi kwamba lebo yake itafunguliwa tena wakati mambo yatakapokuwa sawa, kwani kuna miradi mingi ambayo ilikuwa kwenye lebo yake.