logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Huwezi kupoteza ambacho hukuwa nacho,'Somo kuu Amber Ray alijifunza kufuatia kifo cha rafikiye

Kwa hiyo ameahidi kuishi maisha yake kikamilifu, akieleza kuwa tayari kuwasumbua watu wengi.

image
na Radio Jambo

Burudani23 December 2021 - 09:07

Muhtasari


  • Somo kuu Amberay alijifunza kufuatia kifo cha rafikiye

Mwanasosholaiti mwenye utata Faith Makau almaarufu Amber Ray ametumia ukurasa wake wa Instagram kushiriki kile amejifunza kufuatia kifo cha rafiki yake, Empresal Sally.

Kulingana naye, Amegundua hakuna mtu anayeweza kupoteza asichonacho, akiongeza zaidi kuwa kupoteza rafiki kumemkumbusha umuhimu wa maisha na kwamba yeye pia atakufa siku moja.

Kwa hiyo ameahidi kuishi maisha yake kikamilifu, akieleza kuwa tayari kuwasumbua watu wengi.

Kifo cha Empressal kilipokewa kwa hisia tofauti, wengine wakidai alifariki duniakwa ajili ya kudungwa sindano ya kubadilisha ngozi yake.

Akijibu hili, Amber Ray aliwataka wanablogu kuacha kueneza hadithi za uongo kuhusu rafiki yake.

"Somo kubwa kutoka kwa kupoteza mtu wa karibu nami ni; Huwezi kupoteza kile ambacho hukuwa nacho hapo kwanza. Maisha yaliyopotea ni maisha yenyewe yanakukumbusha kuwa ingawa uko njiani kutoka, bado uko hapa! Bado niko hapa! Sasa nitaishi kama sijawahi hapo awali kwa sababu najua sasa kwamba siku moja nitaondoka na baada ya muda kusahauliwa na wengi. Wakati huo huo, nitawasumbua kwa njia hata mimi bado sielewi. Lakini kwanza, wacha nirudishe ngozi yangu kwenye mstari 😉…. Nitaishi hata kwa wale wasioweza."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved