Desemba ndio mwezi mzito zaidi kwangu-Lillian Muli asema,akumbuka maumivu ya kufiwa na baba yake

Muhtasari
  • Leo, pia amefichua changamoto nyingine anayopambana nayo, kiwewe cha kufiwa na mpendwa
lilian muli
lilian muli

Lillian Muli ni mmoja wa wanahabari maarufu nchini Kenya. Kwa sasa yeye ni mfanyakazi wa Citizen TV inayomilikiwa na Royal Media Services kama mtangazaji wa habari.

Licha ya umaarufu huo, mama huyo wa watoto wawili hajabahatika kuhusiana na mapenzi. Miaka michache iliyopita, alitalikiana na mumewe ambaye alimtuhumu kuwa mnyanyasaji na mpenda wanawake.

Leo, pia amefichua changamoto nyingine anayopambana nayo, kiwewe cha kufiwa na mpendwa.

Kulingana naye, Desemba ndio mwezi wake mbaya zaidi, kwani inamkumbusha kuhusu kifo cha babake.

Hata hivyo, alisema kwamba Krismasi ya mwaka huu huenda ikawa tofauti, kwani baadhi ya marafiki na jamaa zake wamekuwa hapo kwa ajili yake.

Lillian mwenye shukrani alieleza jinsi ambavyo ametiwa nguvu baada ya kutiwa moyo kuishi maisha bora zaidi.

"Ninawashukuru watu ambao wamekuwa maishani mwangu wakati mzuri na mbaya , leo nilikunywa kifungua kinywa na rafiki yangu mwenye moyo mwema duniani

Leo mmoja wa dada wa rafiki yangu ambaye aliaga dunia mwaka jana, alinipigia simu na kunihamasisha na nguvu yake, mwingine amenipigia leo na kuona jinsi ninavyoendelea

Mwezi wa Desemba ndio mwezi mzito zaidi kwangu, na umekuwa kwa maana unanikumbusha nilivyompoteza baba yangu, sijui huwa nasikia aje kuhusu krismasi lakini namshukuru Mungu kwa zawadi."