'Leo nitukane mpaka Ile ya ndani,'Akothee awaambia mashabiki wake

Muhtasari
  • Akothee awapa mashaiki wake fursa ya kumtusi
  • Aliongeza na kuwaambia kwamba anawataka haswa wale ambao wamekata tamaa na hawana mahali pa kumwaga mafadhaiko yao
Esther Akoth

Mjasirimali maarufu Esther Akoth almaarufu Akothee ​​alichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa instagram akiwapa wafuasi wake fursa ya kumtusi.

Kulingana naye alisema kuwa anawapa mashabiki wake wote nafasi ya kumtukana akiwataka wasiogope kwa sababu hatawapa block, lakini atawajibu vyema.

Aliongeza na kuwaambia kwamba anawataka haswa wale ambao wamekata tamaa na hawana mahali pa kumwaga mafadhaiko yao.

Chapisho hili lilivutia hisia za Wakenya ambapo lilikuwa na zaidi ya matusi elfu mbili.

"Leo ni siku ya matusi kwa ajili yetu nataka kuwapa mashabiki wangu wote fursa ya kunitukana, tafadhali usiogope, sitawapa block, lakini nitahudhuria kwa matusi.

Hasa wale ambao wanasumbuliwa na hawana wapi kumwaga mashaka yao 🤣 kuleta hapa mtoto

Leo NitUkane Mpaka Ile Ya Ndaniiiiii, NDANIII. Usikie Viziri. Hii ndio krisnas yangu kwa kama shabiki wangu. Baby Matusi tafadhali 🤣💋," Aliandika Akothee.

Haya a si wadau mmepewa fursa na msanii huyo ya kumtusi vile mnavyotaka.