Nisipate picha mmejipiga kwa compound yangu social media-Akothee awaonya binti zake

Muhtasari
  • Akothee awaonya binti zake dhidi ya kupakia picha za nyumba yake mitandaoni
Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Image: Instagram

Esther Akoth almaarufu madam boss Akothee ni sosholaiti Mkenya mwenye utata anayejulikana kwa kuishi maisha ya akifahari.

Yeye ni mama wa watoto watano na miongoni mwa watu mashuhuri ambao wametoka kwenye shida hadi kuwa tajiri kupitia kwa bidii ya kazi yake.

Siku ya JUmamosi  Akothee alitumia mitandao ya kijamii kuchapisha video akifurahia Krismasi katika boma lake.

Katika video hiyo mwimbaji huyo alikasirishwa na binti zake kwa kukataa kupika chakula chochote wakimsubiri apike na kuwahudumia.

Badala yake walikuwa wakifurahia kwenye bwawa wakinywa mvinyo huku wakimuamuru Akothee awaagize chakula kama bado hajapika.

Akothee hakuweza kuendelea nao alianza kuwafukuza akiwaambia wakome kujivinjari 'slaying' katika boma lake.

 Hata aliwaonya dhidi ya kupiga picha kutoka kwa boma lake na kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii kwani atawaanika vibaya na kuwaweka aibu kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

" Msikuje kwangu kuslay mkipiga picha in the name afternoon vibes . Kwendeni huko bora nisipate Picha Mmejipiga Kwa compound Yangu social media nitawatusi," Akothee aliwaambia binti zake.