Bahati na Diana Marua wamfariji Mama Mueni baada yake kulazwa hospitalini

Muhtasari

• Bahati alimtakia afueni ya haraka  mama huyo wa binti yake huku akiwasihi mashabiki wake kumkumbuka kwa maombi  katika kipindi hiki kigumu.

•Siku kadhaa zilizopita Yvette alifahamisha mashabiki wake kwamba hangeweza kufurahia Krismasi vizuri kwani alikuwa anaugua.

Diana Marua, Bahati, Yvette Obura
Diana Marua, Bahati, Yvette Obura
Image: INSTAGRAM

Baby Mama wa Bahati,  Bi Yvette Obura amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kushambuliwa  na ugonjwa usiothibitishwa.

Siku ya Ahamisi Yvette alitumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kwamba amelazwa huku akipakia picha iliyoonyesha akiwa amelala katika kitanda cha hospitali na kuvalia mavazi ya wagonjwa.

Mama huyo wa binti mmoja alimshukuru aliyekuwa mpenzi wake, Bahati pamoja na mkewe Diana Marua kwa kumtembelea na kumfariji anapoendelea kupokea matibabu.

"Shukran @bahatikenya na @diana_marua kwa kuja. Shukran pia kwa famila na marafiki kwa kuja na kufanya mawasiliano" Yvette aliandika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati alimtakia afueni ya haraka  mama huyo wa binti yake huku akiwasihi mashabiki wake kumkumbuka kwa maombi  katika kipindi hiki kigumu.

Diana Marua pia alikuwa amemwandikia Yvette ujumbe akimuombea afueni ya haraka.

"Pona haraka Mama Mueni @yvette_obura. Kupona ni sehemu yako katika jina la Yesu" Diana aliandika.

Siku kadhaa zilizopita Yvette alifahamisha mashabiki wake kwamba hangeweza kufurahia Krismasi vizuri kwani alikuwa anaugua.

"Siamini ni mimi sijakula kuku juu ya ugonjwa. Macho yangu yanaonyesha jinsi nilivyo mgonnjwa" Yvette alisema.

Yvette na Bahati wana mtoto mmoja wa kike anayeahamika kama Mueni ambaye walipata kabla ya mwanamuziki huyo kujitosa kwenye mahusiano na Diana Marua.