logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Kila jambo linawezekana,'Ujumbe wa Ommy Dimpoz wa kutia moyo kwa mashabiki mwaka mpya

Pia ameongeza kusema jambo la muhimu maishani ni kumshukuru Mungu kwa uzima na afya njema.

image
na Radio Jambo

Habari03 January 2022 - 09:14

Muhtasari


  • Ujumbe wa Ommy Dimpoz wa kutia moyo kwa mashabiki mwaka mpya
images ommy

Ommy Dimpoz ni mmoja wa wasanii wa muziki wanaotafutwa sana Afrika Mashariki.

Sawa na watu wengine maarufu, Ommy Dimpoz kupitia mitandao ya kijamii amewatakia mashabiki wake heri ya mwaka mpya na ameshiriki ujumbe wa kutia moyo.

Alisema alipata mengi ya kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita wa 2021 ingawa kulikuwa na changamoto kadhaa.

Pia ameongeza kusema jambo la muhimu maishani ni kumshukuru Mungu kwa uzima na afya njema.

"Bismillaah: Yapo Mengi Ya Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Mwaka Uliopita Yapo Malengo Yaliyofanikiwa na ipo mitihani Ambayo pengine imeleta kikwazo kwenye Malengo yetu.Jambo la Muhimu ni Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Afya na Uzima na kuwaombea wale Walio kitandani Waweze kuinuka," Ommy Aliandika.

Kuhusu masuala ya uchapakazi na ustahimilivu, Ommy Dimpoz amesema kuwa amejifunza kutoka kwa walio mbele yake aidha kifedha kwamba kila kitu kinawezekana ukiweka kazi na kubaki. umakini kwa sababu hakuna mtu aliyewahi kwenda shule ya maisha.

"Kitu nilichojifunza na Nachoendelea kujifunza kwa Walionizidi iwe kiakili ama ki Fedha ni kuwa kila jambo linawezekana

Cha muhimu ni kupambania ndoto zetu na kuwa focused Hakuna aliyesomea Maisha,Ukiwa na Nidhamu na Juhudi huku ukimuomba Mungu basi jua Wakati wako utafika na Riziki yako itaongezeka wala tusioneane Choyo pale Mwenzako anapopiga hatua,tusikate tamaa wala kuhuzunika pale unapopata vikwazo kwenye utafutaji wetu kwani hata mitume ilipigwa vita na kuchukiwa itakuwa wewe mtoto wa Binti Saidi 😃."

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved