'Wacha kutafuta kiki ni 2022,' Willy Paul amwambia Ringtone baada ya madai ameiba kibao chake

Muhtasari
  • Willy Paul amshauri Ringtone kuacha kutafuta kiki
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Msanii Willy Pail almaarufu Pozze ameonekana kugadhabishwa na matamshi yake msanii wa nyimbo za injili Ringtone.

Hii ni baada ya Ringtone kudai kwamba kibao chake Willy Paul kinachofahamika kama 'Atoti Jaber' alikiiba kutoka kwake.

Kupitia kawenye ukurasa wake wa instagram Paul alimwambia msanii huyo kwamba kibao hicho hakijawahi kuwa cha inili na kwamba huu ni mwaka mpya anapaswa kuacha kutafuta kiki.

Pia alimhakikishia kwamba anampa heshima kwani ni yeye alimtangulia katika tasnia ya usanii.

"Wale mnaojua Ringtone mnajua yeye ni mtu wa aina gani.. Ndugu yangu tafadhali acha kuwaambia marafiki zako kuwa nilikuibia wimbo wa atotijaber. Haijawahi kuwa wimbo wa injili, inatosha na wacha ktafuta kiki kaka, Ni 2022, mwanzo mpya. Ninakupenda na kukuheshimu kama kaka mkubwa aliyekuja kwenye tasnia hii kabla yangu," Alisema Pozze.