'Bill inapanda excess,'Sandra Dacha afichua Akuku Danger anaendelea vyema,licha ya bili ya hospitali kuongezeka

Muhtasari
  • Dacha hata amefichua kwamba Akuku kwa mara ya kwanza aliomba chakula baada ya hali yake kuonekana kuwa nzuri
Image: INSTAGRAM/ SANDRA DACHA

Mcheshi wa Kipindi cha Churchill Akuku Danger yuko hospotalini kwa siku ya saba hii leo  katika Hospitali ya Nairobi West chini ya Chumba cha Wagonjwa Mahututi.

Tofauti na hali yake ya awali ya afya, mcheshi huyo anapata nafuu taratibu kama ilivyofichuliwa na rafiki yake Sandra Dacha.

Kwa kweli, Dacha hata amefichua kwamba Akuku kwa mara ya kwanza aliomba chakula baada ya hali yake kuonekana kuwa nzuri.

"Akuku Danger hatimaye ameomba chakula, Haleluya. Njaa sio kitu kizuri." Dacha alifichua.

Hata hivyo, licha ya uboreshaji ulioshuhudiwa, Dacha ameambulia changamoto moja tu katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi.

Kulingana na Dacha, bili ya hospitali imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika kipindi kifupi na ndani ya siku sita; bili ya matibabu sasa inafikia Ksh.1.5 milioni.

"Bill inapanda excess wuueh, imekuwa siku sita na tuko milioni 1.5." Dacha alisema.

Hata hivyo, hakupata wasiwasi mwingi kuhusu hilo lakini alifurahi tu kwamba Akuku alikuwa akipata nafuu.

Aidha, Dacha alitoa shukrani zake kwa mashabiki wote walioshiriki katika michango na maombi kwa ajili ya Akuku Danger.

Alipohitimisha, aliwaomba Wakenya kuendelea nao hadi tabu yao ikamilike.