Utaanguka! Bobi Wine amhutubia Museveni katika wimbo mpya

Muhtasari

•Amesema kwamba  alilazimika kufichua uhalifu uliofanywa chini ya utawala wa rais ndio sababu picha zilizotumika kwenye video zinatisha.

Image: EPA

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mwanamuziki Bobi Wine ameachia wimbo mpya kwa jina Ogenda, neno la Kiganda linalomaanisha "Utaanguka".

Wimbo huo unamlenga Rais Yoweri Museveni moja kwa moja kwa sababu amekiuka ahadi yake kuleta demokrasia nchini, anasema.

Bobi Wine ameambia BBC  kwamba alilazimika kufichua uhalifu uliofanywa chini ya utawala wa rais ndio sababu picha zilizotumika kwenye video zinatisha.

"Utawala nchini Uganda umewekeza pesa nyingi kuficha ukatili huo," alisema.

Bobi Wine alisema vyombo vya habari nchini Uganda vimezimwa na njia pekee ya kufichua uozo huo ni kupitia muziki.

"Haki inaweza kupatikana pale tu tunapofichua uhalifu, ndiyo maana tunaendelea kuuibua, hiyo ndiyo njia pekee tunayoweza kupambana nayo," alisema.