Achana na watu wanaokufanya ujiulize thamani yako- Michelle Ntalami

Muhtasari
  • Michelle Ntalami awashauri mashabiki wake waachane na watu wanaowafanya wajiulize thamani yao
Michelle Ntalami
Image: Hisani

Michelle Ntalami amekuwa akitumia  akaunti yake ya Instagram kutangamana na mashabiki wake,huku akipakia chapisho za kutia moyo kwa mashabiki.

Mjasirimali huyo amewashauri mashabiki wake kukumbatia mwaka mpya.

Michelle anawakatisha tamaa mashabiki wake kutokana na kutarajia mabadiliko ya furaha na laini.

Kilichozua shauku zaidi ni pale alipofichua kwamba alilazimika kuacha kufuata watu wenye sumu. Ntalami alidokeza kuwa watu kama hao wanaweza kukufanya utilie shaka thamani yako.

Mitchell anawahakikishia mashabiki wake mwaka wenye baraka ikiwa watajitenga na watu ambao walifanya mwaka wao uliopita kuwa mgumu.

Alisema huo ni mwanzo mzuri kuelekea kufurahia mwaka wenye matunda.

"2022 haitakuwa bora kwa maana kalenda imebadilika, lakini ukianza kufuta hizo jumbe zenye sumu,na kuacha kufuata watu ambao watafamya ujiulize thamana yako

Na kuachana na wao kabisa wale waliofanya mwaka wa 2021 kuwa mgumu zaidi kwako kuliko vyenye ulikuwa, huo ni mwanzo mzuri," Aliandika MItchell.