Namtakia kila la kheri maishani mwake,'DJ Kalonje asema baada ya kuachana na mpenzi wake

Muhtasari
  • Mcheza santuri DJ Kalonje waachana na mpenzi wake
DJ Kalonje na Rachel
Image: DJ Kalonje/INSTAGRAM

Mcheza santuri maarufu nchini, DJ Kalonje kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kutengana kwake na mpenzi wake Rachel.

Kulingana na Kalonje walikubaliana kuachana kama watu wazima bali kumbukumbu za wakati ambao walitumia pamoja watabaki nazo.

Aidha alisema kwamba katika dunia lazima mambo yote mazuri yafikie mwisho.

Ujumbe wake ulisoma;

"Heri ya 2022 jamaa! Katika maisha mambo yote mazuri lazima yafike mwisho, hata wakati wa kushangaza zaidi na marafiki na wapendwa. Kilicho muhimu ni kumbukumbu zinazoundwa na pia masomo yaliyopatikana.

Ningependa kusema kuwa mimi na Rachel aka Laquina tumeamua kila mmoja kwenda zake. Kwa heshima kwa kila mmoja juhudi za baadaye.

Namtakia kila la kheri maishani tunapoanza safari tofauti.

Upendo mmoja!DJ KALONJE," Aliandika Kalonje.