'Amekaribishwa kutembelea mtoto wangu,'Vera Sidika asema haya kuhusu Otile Brown

Muhtasari
  • Vera Sidika kwa mara ya kwanza amezungumza kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake wa zamani Otile Brown

Vera Sidika kwa mara ya kwanza amezungumza kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake wa zamani Otile Brown.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa Instagram Vera alisema yeye na Otile sio marafiki na hata hawaongei ila kwa upande wake hana kinyongo na Otile Brown na Otile yuko huru kuja kumtembelea na kuona mtoto wake Asia.

Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza kama angekubali Otile kuona mwanawe iwapo siku moja atakuja.

"Huwa siweki kinyongo, kwa hivyo ndio amekaribishwa kunitembelea kama anataka, sio marafiki na baba Asia lakini walipatana mara moja kitambo," Alijibu Vera.

Otile na Vera walikuwa wapenzi, na hata Wakenya wengi walikuwa wametabiri, kwamba wawili hao wataoana.

Ingawa mambo hayakuenda walivyokuwwa wanataka na uhusiano huo ulidumu kwa mwaka mmoja tu na wakaachana.

Otile akaendelea na pia Vera akasonga mbele na kwa sasa ana uhus wa ianokimapenzi na Brown Mauzo na wanaishi maisha ya furaha sana.

Vera pia alisema kuwa Otile na Brown Mauzo si marafiki, ingawa wamewahi kuwa pamoja katika mazingira ya kazi.

Pia alisema hana chuki wala kinyngo na Otile Brown, haya basi Otile jua kwamba umekaribishwa nyumbani kwa Vera 

Vera alisema baada ya kuachana na Otile hajawahi kua kumtembelea.