Mimi mwenyewe kabla mume nilikua nimezoea kujituma na kushika hela yangu-Nyota Ndogo

Muhtasari
  • Nyota Ndogo aweka wazi hawezi kumtegemea mumewe kupita kiasi
nyota ndogo
nyota ndogo

Nyota Ndogo amejitokeza waziwazi kuwakomesha watu wanaomwambia aache kazi kwa sababu ameolewa na Mwanamume tajiri.

Nyota Ndogo alisema ni kweli mume wake Nielsen raia wa Uholanzi ana pesa nyingi, lakini kwake tangu utotoni amekuwa akitafuta pesa peke yake na kula pesa anazohangaika nazo.

Nyota Ndogo pia alisema kwamba, si vizuri kupumzika na kumtegemea mpenzi wake tajiri kupita kiasi, kwa sababu hakuna aijuaye kesho labda anaweza kufa, akabaki na hakuna kitu, na kulazimishwa kuanza maisha tena kutoka sifuri.

Nyota Ndogo alisema kuwa amefungua hoteli mpya huko Voi na Wakenya wanapaswa kumuunga mkono kwa kwenda kula hotelini.

"Nikiwa Jikoni uwa akili inafikiria kazi tu. Wengi wananiuliza kwanini najisumbua na nimeolewa na mtu mwenye hela but kitu watu hawajui ni kuna Leo na kesho

Wengi ambao wameolewa na watu wenye pesa hujisahau wakaiona Kama dunia wameibeba mkononi

Mimi mwenyewe kabla mume nilikua nimezoea kujituma na kushika hela yangu hata kama ni kidogo najivunia kilicho changu

Wanaosema nikae nisifanye kazi nimeolewa na mume mwenye pesa kumbukeni kuna kufa anaeza akafa yeye ama mimi mbele itokee ameondoka yeye mbele na mimi nimejizoesha kukaa fwaaaa nangoja kulishwa,kuvishwa na kusomeshewa watoto;si ndo naanza kuchekwa mimi.Si ndo ntasimangwa mimi

Si ndo ntaambiwa alikua yuaringa Amerindian zero.Maana wengi tunawaona waliokua na maisha mazuri baada ya kuondokewa wanapata shida kwasababu walikua hawafanyi chochote cha kujitegemea.Niacheni jamani napenda ninachokifanya.Asanteni."