Ulikuwa unawachapa kama mbwa-KRG The Don amuonya dada ya aliyekuwa mkewe dhidi ya kuwatembelea wanawe

Muhtasari
  • KRG The Don amuonya dada ya aliyekuwa mkewe dhidi ya kuwatembelea wanawe
Rappa KRG the Don
Image: INSTAGRAM/KRG

Msanii KRG The Don amezua hisia tofauti mitandaoni baada ya, kuwa na vita za maneno na dada ya aliyekuwa mke wake.

Katika chapisho lake la hivi karibuni, Krg ametoa onyo kwa Racheal dhidi ya kuwatembelea na kuwasumbua wanawe wawili Neville na Naem wakiwa shuleni.

Krg amemwambia Racheal kwamba kila anapomtembelea mtoto wake Riyah shuleni, asiwahi kuwa karibu na wanawe, kwa sababu anawatia kiwewe.

Kulingana na msanii huyo kuna wakati ambao alikuwa anawatesa watoto wake kwa kuwachapa kama mbwa, ihali hajawahi lipiza kisasi.

Zaidi ya yote alimkumbusha jinsi alivyo msaidia mwanawe wakati alikuwa na matatizo ya pesa.

"Mtu yeyote ambaye anajaribu kuwachanganya watoto wangu anakuwa adui namba moja kwangu Racheal Kiruthi !!!!!! pata onyo, wakati mwingine utapokuwa umeenda kumtembelea mwanao shuleni usiende karibu na watoto wangu, tena

Zingatia familia yako na acha familia yangu iwe na amani ambayo tunafurahia baada ya kukabiliana na upuuzi wote ambao wewe na familia yako mlitufanya tupitie….

Ulipokuwa unawatesa watoto wangu kwa kuwapiga kama mbwa na kuwalisha noodles  na mala na Ugali kwa mwezi 1 mfululizo hukujua kuwa ni watoto wa dada yako?

Ama kwa sababu dada yako alipokuwa makini na wapenzi wake na akawaacha watoto wangu kwa huruma yako kwa siku kadhaa ulifikiri sitawahi kuokoa watoto wangu?

Niwakumbushe tu kwa watoto wangu naweza kuwa mkatili sana zile kofi ulikula 12th April 2021 ni kidogo

Wakati mwingine tukikutana utajua haujui usicheke na Bughaaa," Aliandika KRG.

Krg aliendelea na kumwambia kwamba ikiwa hatazingatia maonyo yake, basi atamshughulikia yeye binafsi na, ataendelea na kumpiga kofi mbaya sana.

"Nakushauri ujikite katika kumpotosha dada yako Ndio asiwahijua ukweli wa jinsi unavyomzungumzia nyuma yake na ulichokuwa unawafanyia watoto wangu huko Nys

Kweli Asante ya punda ni mateke nilikaa na binti yako (Riyah) zaidi ya miaka miwili na sijawahi kumnyanyasa wala kukuomba chochote kwa sababu nilijua hauko sawa kifedha lakini naskianga ulikua unatumia dada yako pesa abapo  alikuwa akitoa kila kitu kwa wakati mmoja….

Kama unajipenda hata kidogo tafadhali kaa mbali na watoto wangu kabisa ama utajua kofi za Bughaaa hukata sura za watu kama panga ( nenda usimame mbele ya kioo kwa makumbuko ya haraka)

Sitanyamaza na kuona watoto wangu wakipitia kiwewe tena kwa sababu yako…. Cheza mbali sana na family yangu!!!"