Nampeza! Wambui Collymore amtakia marehemu mumewe heri za siku ya kuzaliwa

Muhtasari

•Wambui amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Safaricom Michael Joseph  kwa kumtambulisha Collymore maishani mwake.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Bob Collymore na mkewe Wambui Kamiru-Collymore katika hafla ya awali.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Bob Collymore na mkewe Wambui Kamiru-Collymore katika hafla ya awali.
Image: MAKTABA

Bi Wambui Kamiru Collymore amemtakia marehemu mume wake Bob Collymore heri za siku ya kuzaliwa.

Wambui ametumia ukurasa wake wa Twitter kumsherehekea bosi huyo wa zamani wa Safaricom takriban miaka miwili unusu tangu kuaga kwake.

"Heri za kuzaliwa Bw. Collymore @bobcollymore" Wambui ameandika na kuambatisha ujumbe wake na picha ya mume wake marehemu.

Wambui amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Safaricom Michael Joseph  kwa kumtambulisha Collymore maishani mwake. 

Joseph alikuwa ametakia marehemu Collymore heri za siku ya kuzaliwa na kusema kwamba anampeza sana.

"Capricon mwenzangu! Nampeza sana" Michael Joseph aliandika.

Wambui alikiri kwamba anampeza sana marehemu mumewe pia.

"Nimemkumbuka pia MJ. Asante kwa kumleta katika maisha yangu. Na, kwa kweli, siku ya kuzaliwa yenye furaha kwako pia! " Wambui alimjibu Michael Joseph.

Hivi leo (Januari 13) Collymore angekuwa anasherehekea kuhitimu miaka 63 iwapo bado angekuwa hai.

Collymore aliaga duniua mnamo Julai 1, 2019 akiwa nyumbani kwake Kitusuru baada ya kuugua saratani kwa kipindi kirefu.

Aliaga akiwa na umri wa miaka 61 na kuacha mjane mmoja na watoto wanne.