Sitawahi weka mwanamume wangu mitandaoni- Adai Lilian Muli

Muhtasari
  • Lilian pia alizungumza kuhusu maisha yake ya hivi majuzi ya mapenzi akisema ana furaha.
lilian muli
lilian muli

Mwanahabari maarufu Lilian Muli, akiwa kwenye mahojiano na Mpasho  amedai na kukiri kwamba hatawahi pakia mwanamume wake mitandaoni.

"Hatuko kwenye uhusiano na kila mtu tunayepiga naye picha. Mimi ni mtu wa kijamii na napenda kupata marafiki wapya kila mahali ninapoenda.

Naomba usiwaze kuhusu nani ni mpenzi wangu na nani si inaumiza watu wasio na hatia hasa wale wanaowapenda watu unaodai wako kwenye mahusiano ambayo hayapo,” alisema.

Lilian pia alizungumza kuhusu maisha yake ya hivi majuzi ya mapenzi akisema ana furaha.

"Nina furaha kuliko nilivyowahi kuwa. Nipo mahali pazuri na niamini nisingeweza kuweka picha ya mtu wangu."

Alipoulizwa ikiwa hadithi ghushi zinaathiri maisha yake ya kijamii na kama anaogopa kutuma wanaume kwenye mitandao yake ya kijamii, Lilian alisema watu wanapaswa kuheshimu mitandao ya watu.

"Jaribu kutoona vitu ambavyo vipo akilini mwako tu. Sidhani ni sawa kuwaunganisha watu isipokuwa wamesema wazi kuwa wako pamoja," alisema.