Alinipa 'block' baada ya kumfanya awe staa-Magix Enga afichua hawazungumzi na Arrow Bwoy

Muhtasari
  • Magix Enga afichua hawazungumzi na Arrow Bwoy
  • Enga anafahamika sana nchini kwani alianya muziki wa Gengetone kujulikana sana nchini
Magix Enga
Magix Enga
Image: Instagram

Bila shaka tasnia ya muziki, inainuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine, licha ya changamoto ambazo wasanii wanapitia nchini.

Mzalishaji maarufu nchini Magix Enga akiwa kwenye mahojiano, alifichua jinsi alivyokuwa maarufu baada ya kujiunga na Illuminati na jinsi alivyoanguka.

Enga anafahamika sana nchini kwani alianya muziki wa Gengetone kujulikana sana nchini.

Pia akiwa kwenye mahojiano alifichua kwamba hawana uhusiano mzuri na msanii Arrow Bwoy, huku akisema kwamba amewasaidia wasanii wengi lakini hawana shukrani.

"Nilikuwa wa bei ghali kwa njia ambazo nilitumia kupata pesa, niliwasaidia wasanii wengi kujulikana lakini wasanii wakenya hawana shukrani

Msanii kamaArrow Bwoy amenipa block na sikumkosea mimi,nilimwabia niaje ndugu yangu hukulipa kijana wangu session, anakula kwangu namfanyia kila kitu simumpe ata kama ni lefu 5,000 ya chakula akaniblock, nilimfanya ajulikana katika tasnia ya muziki," Alidai Magix Enga.