Akothee afichua sababu ya kununua simu na kadi ya simu mpya kila mwaka

Muhtasari
  • Akothee afichua sababu ya kununua simu na kadi ya simu mpya kila mwaka
Esther Akoth

Msanii tajika Esther Akoth almaarufu Akothee kupitia kwenye ukura wake wa instaram amefichua sababu kuu ya kubadilisha kadi ya simu na simu mpya kila mwaka.

Akothee anafahamika sana kwa ajili ya bidii ya kazi yake, na maisha anayoishi ya kifahari.

Kulingana na Akothee sababu yake kuu ya kununua simu mpya kila mwaka ni kujiepusha na mahusiano yenye sumu, na pia hapendi kuwapa watu block.

"Mimi hununua simu mpya na laini mpya kila mwaka, ili tu kuacha nishati hasi, yenye sumu niliyokusanya katika mwaka!

Sijui baadhi yenu mnawezaje kukabiliana na laini moja ambayo kila mtu anapiga 🤔🤔🤔 Pia sijui watu wachache ninaowapa namba yangu wanaishiaje kuitoa 🤔 Kwa vile sijui kujifanya na kuwapa block najihisi kukosa heshima, nasogea tu harakaharaka. Kwa mstari mpya 🤣🤣🤣🤣🤣 Inaitwa Maisha Usafi," Akothee Aliandik