logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kucheatiwa kunauma sana-Jacquline Wolper

Kuongeza kuwa kudanganywa kunaumiza sana haswa ikiwa ni mtu anayekupenda.

image
na Radio Jambo

Habari24 January 2022 - 11:22

Muhtasari


  • Wolper hata hivyo amesema hata akipata ujumbe kuwa kuna mtu amelala na mwanamume wake hatamuacha
  • Kuongeza kuwa kudanganywa kunaumiza sana haswa ikiwa ni mtu anayekupenda
wolper-696x870

Wolper ambaye ni mwanasosholaiti wa Tanzania na ambaye amewahi kuwa mpenzi wa msanii Harmonie kupitia kwenye ukurasa wake amesema kudanganywa na mtu umpendaye inauma sana.

Wolper aliendelea na maisha yake na kwa sasa yupo kwenye mahusiano thabiti na mwanamume ambaye anadai kumpenda sana ambaye pia anatokea kuwa baba wa mtoto wake ambaye amefanana naye.

Wolper hata hivyo amesema hata akipata ujumbe kuwa kuna mtu amelala na mwanamume wake hatamuacha.

Kuongeza kuwa kudanganywa kunaumiza sana haswa ikiwa ni mtu anayekupenda.

Alisema kwamba hii ilikuwa baada ya rafiki yake kuchezwa na mwanamume wake na kumshauri rafiki huyo kumwacha mwanamume huyo.

Akisema kuwa licha ya kufanya hivyo, hawezi kumuacha mwanamume wake kwa kudanganya.

Katika hilo anaweza kumuacha tu ikiwa ana ushahidi na wiki moja baadaye atamtambulisha mwanaume wake mpya.

"Nilishaa sema huu usemi,lakini ningegundua nilikuwa na njaa hiyo siku sikula vizuri kiukweliKucheatiwa kunauma sana kwa mtu unayempenda nakumuamini nimegundua hiki kitu baada ya mdogo wangu kunambia bwanake kaweka paswad kwenye simu nikwamwambia anakucheat lazma umuache

Sasa vip nimkute na mtu tu nisimuache siwezi narudia maneno yangu nikiwa nimeshiba pilau siwezi nitaachana nae siku nikimkuta  nauakika ninao na baada ya wili nitamtambulisha baba wa kambo," Aliandika Wolper.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved