'Usitumie picha zetu bila idhini,'Mulamwah amuonya DJ wake Diamond baada ya kufanya haya

Muhtasari
  • Mulamwah amuonya DJ wake Diamond baada ya kutumia picha yake bila idhini
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mcheshi maarufu wa Kenya David Oyando almaarufu Mulamwah hajafurahia, baada ya kubainika kuwa picha yake ya awali akiwa na mpenzi wake wa zamani Carrol Sonie ilitumiwa isivyo haki kwa ubinafsi.

Alifichua haya kupitia hadithi zake za insta kwa kuweka picha ya skrini yake, ambapo ilikuwa wazi kuwa ni DJ wa Diamond Platnum, moniker Romy Jons ambaye alitumia picha hiyokutangaza biashara ambayo inajishughulisha na bidhaa zinazoongezanguvu za kiume kwa wanaume.

Kulingana na chapisho la Romy Jons ambaye pia ni Mkurugenzi wa Muziki wa Wasafi Media, ilikuwa wazi kuwa picha hiyo ilikuwa ya Mulamwah na Carrol Sonie walipopiga wakati,Carol alikuwa mjamzito.

Hii ilikuwa wiki chache tu kabla ya binti yao Keilah Oyando kuzaliwa haswa.

Hata hivyo, katika maelezo yake, mwanamume huyo mcheshi alifoka na kumuonya DJ kwa kutumia picha hiyo kwa nia mbaya bila hata kuomba ruhusa yao.

Alimtaka zaidi kuifuta:

"Kakangu @romyjons naomba usizitumie picha zetu kwa matangazo ya kibiashara ila idhini, haswa mswala ya ngono na nguvu za kiume.Deliti unatuzalilisha," Aliandika Mulamwah.