Msanii kutoka bongo, Rayvanny almaarufu Chui amesema kwamba anakwenda kuachia EP yake ya kwanza ya 2022 mnamo tarehe 10/02/2022.
Kulingana na picha ambayo ameachia kwenye ukurasa wake wa Instagram, EP hiyo yenye title ya FLOWERS II itakuwa na ngoma tisa huku ikishuhudia kolabo na wasanii tofauti ndani ya Tanzania na mataifa mengine ya nje.
Miongoni mwa wasanii watakaofankiwa kuingia katika EP hiyo ni pamoja na: Nadia Mukami, Guchi, Ray C, Marioo, Clyde, Roki pamoja na Zuchu.
‘Post hii inajiri siku chache tu baada ya ngoma yake ya #mamtetema aliyomshirikisha msanii Maluma kutoka Colombia kufanya vizuri katika chati tofauti za taifa la Mexico.
Kulingana na wasanii ambao wamehusishwa humo, sni bayana kwamba itakuwa EP ambayo itatetemesha mawimbi ya burudani ndani ya Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki kwa ujumla.