Mwimbaji wa Tanzania Zuchu amekuwa akivuma tangu alipodaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi wake, mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi Diamond Platinumz.
Zuchu alijiunga na Wasafi mwaka 2020 na amekuwa akitoa nyimbo zinazovuma. Kipaji chake kilimfanya kufikia msanii bora wa kike Afrika Mashariki katika tuzo mbalimbali.
Mbali na tuzo hizo, Zuchu pia ndiye msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kupata watazamaji zaidi ya milioni moja kwenye YouTube.
Zuchu alikuwa ameweka maisha yake ya mapenzi kuwa siri hivi majuzi ilipodaiwa kuwa alikuwa akichumbiana na Diamond.
Uhusiano wao bado haujawa wazi kwani wengi wanadai ni kwa ajili ya kustaajabisha hadharani kitu ambacho wasanii wengi hufanya wanapotaka kutoa wimbo au albamu.
Wamekuwa wakituma picha na video za kila mmoja wao. Pia wamekuwa wakiwaweka mashabiki wao wasiwasi kwani waliahidi harusi yao itafanyika tarehe 14 Februari.
Hii hata hivyo imebadilika kwani Zuchu ameweka wazi. Katika mahojiano na Wasafi fm leo asubuhi mwanadada huyo mwenye kipaji alifichua kuwa tarehe 14 Februari atakuwa na kipindi na sio harusi.
"Kuhusu Tarehe 14/2/2022 ! Kutakua na Show Yangu Kubwaaa sana Siku ya Valentine Day Na Ndio maana Watu wengi wemenipost kunitakia kila la Kheri akiwemo Mama Yangu Mzazi ila kutakuwa na SUPRAIZI," Zuchu Alizungumza.
Aidha alisema kwamba staa wa bngo Diamond ni bosi wake na wala sio mpenzi wake, na atasalia kuwa bosi wake siku zote.
Lakini swali kuu linalosalia bila kujibiwa ni wawili hao kweli ni wapenzi au ni kiki tu wanatafuta?