Kama ilivyoada penye moshi hapakosi moto, tetesi na uvumi za mahusiano baina ya Zuchu na Diamond platinumz zimeonekana kuendelea kuwa ngumzo mitandaoni kila uchao.
Habari za Zuchu kutoka kimapenzi na bosi wake, Diamond Platnumz zimekuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa takribani miezi mitatu.
Zuchu kwenye mahojiano yaliyofanyika Jumatano nchini Tanzania ilibainika picha ambayo ameweka kwenye wallpaper yake si yake ila ya bosi wake, Diamond Platinumz.
Isitoshe,alipofika kwenye kituo hicho cha habari alipokuwa akihojiwa alieleza wazi kuwa Diamond alimpigia simu kuhakikisha kama aliwasili kwenye mahojiano kwa wakati.
Ingawa Zuchu alionekana kukana madai kwamba wanachumbiana na bosi wake, alifichua kuwa siku ya wapendanao atawambia mashabiki wake ukweli kuhusu mahusiano yake.
Ikumbukwe Jumatatu Mamake Zuchu, Khadija Kopa aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia mwanawe ndoa ya furaha huku akieleza hana shaka na maamuzi ya mwanawe.
Zuchu anakaribia kufikisha miaka miwili kwenye lebo ya Wasafi, ambapo ameonekana kupata wafuasi wengi, si kwa mitandao ya kijamii bali pia kwenye youtube.